#Sports

COVID YATIKISA OLYMPICS

Zaidi ya wanariadha 40 katika Michezo ya Olimpiki ya Paris ya 2024 wamepatika kuugua Covid-19 ishara ya ongezeko la visa vya maambukizi hayo ulimwenguni kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni.

WHO ilisema virusi vinavyosababisha Covid-19 bado vinazunguka na nchi zinahitaji kuimarisha mifumo yao ya kukabiliana navyo.

Wanariadha kadhaa wa hadhi ya juu wameugua Covid-19 kwenye Michezo ya Paris.

Muogeleaji wa Uingereza Adam Peaty alipatikana na virusi siku moja baada ya kushinda medali ya fedha katika mbio za mita 100. Mshindi wa medali ya Australia Lani Pallister alijiondoa katika mbio za mita 1500 za wanawake baada ya kuugua.

Takwimu kutoka nchi 84 zinaonyesha kuwa asilimia ya vipimo vya virusi vya SARS-CoV-2 — virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 – imekuwa ikiongezeka kwa wiki kadhaa, alisema Maria Van Kerkhove, mkurugenzi wa kusimamia majanga na kinga WHO.

Imetayarishwa na Nelson Andati

COVID YATIKISA OLYMPICS

CHEPTEGET HAYUPO MBIONI

COVID YATIKISA OLYMPICS

MAFUNZO KWA MAKOCHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *