POLISI 5 KUJUA HATMA YAO YA DHAMANA

Macho yameelekezwa katika mahakama kuu kuona iwapo itawapa dhamana au la maafisa 5 wa polisi waliokuwa wakihudumu katika kituo cha polisi cha Gigiri ambao wanashukiwa kuwasaidia Collins Khalusia na wenzake kutoroka.
Hii ni baada ya upande wa mashtaka hapo jana kuomba wazuiliwe kwa siku 14 zaidi ili kukamilisha uchunguzi dhidi yao.
Watano hao waliosimamishwa kazi na kuzuiliwa, walifikishwa mahakamani hapo jana, mashahidi wakisema Khalusia na wenzake waliondoka katika kituo hicho wakitumia lango kuu huku maafisa wa polisi waliokuwa kwenye zamu wakitazama.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa