TUJU ANAONGOZA MATEMBEZI YA KM 50 KUTAFUTA FEDHA KWA AJILI YA KITUO CHA KIJAMII CHA ICT

Aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri Raphael Tuju ameongoza mamia katika matembezi ya kilomita 50 kuchangisha fedha za kuanzishwa kwa kituo cha kijamii cha ICT katika kijiji cha Ralingo katika kaunti ndogo ya Rarieda.
Matembezi hayo ya mwendo wa saa 8 yalianza kutoka mjini Kisumu na kuishia katika kijiji cha Ralingo, kaunti ndogo ya Rarieda katika Kaunti ya Siaya.
Kulingana naTuju mradi huo unalenga kuwawezesha vijana kujikimu kimaisha kupitia kufanya kazi mtandaoni.
Imetayarishwa na Janice Marete