KIONI AWASUTA WAKOSOAJI

Katibu mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni amepuzilia mbali kauli za baadhi ya viongozi kwamba eneo la Mlima Kenya halifai kulalamika kwani limetengewa nafasi nyingi serikalini.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, Kioni amesema kuwa na kiongozi kutoka eneo hilo haimaniishi kwamba maslahi ya wakazi yameshughulikiwa kikamilifu.
Aidha, ametetea mfumo wa ugavi wa mapato kwa misingi ya idadi ya watu, akisema eneo la mlima Kenya litafaidika pakubwa kupitia mfumo huo.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































