#Local News

WALIMU WAHIMIZWA KUOMBA NAFASI YA KATIBU NA AFISA MKUU MTENDAJI WA TSC

Walimu waliohitimu na ambao wanatimiza vigezo vya uongozi wanahimizwa kuwasilisha maombi ya nafasi ya Katibu na Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC), kufuatia kuondoka kwa Dkt. Nancy Macharia katika muda wa chini ya miezi miwili ijayo.

Waombaji wanatakiwa kuwa raia wa Kenya, wawe na shahada ya elimu, uzoefu wa si chini ya miaka 10 katika elimu, usimamizi au utawala wa umma, na pia kutimiza masharti ya Sura ya 6 ya Katiba ya Kenya.

Fomu za maombi zinapatikana kwenye tovuti rasmi ya TSC na zinapaswa kuwasilishwa katika afisi ya Mwenyekiti wa Tume, huko Upper Hill, Nairobi, kabla ya Jumanne, tarehe 27 Mei 2025.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *