#uncategorized

TUACHE SIASA ZA UKABILA

Mbunge wa kikuyu Kimani Ichungwa amewakashifu viongozi wanaotumia swala la ukabila kuwaunganisha wakaazi wa mlima kenya akisema siasa hizo zilipitwa na wakati.

Wito huo unajiri wakati ambapo naibu wa rais Rigathi Gachagua amekuwa akiendelea na mchakato wa kuwaunganisha viongozi wa eneo la mlima Kenya huku kundi jingine likiongozwa na katibu mkuu wa chama cha jubilee Jeremaya Kioni na Martha Karua wa KNARC kenya likipanga mkutano wa viongozi wa mlima kenya maarufu Limuru 3 ijumaa wiki hii.

Kauli hiyo imetiliwa mkazo na mbunge wa Laikipia mashariki Mwangi Kiunjuri wawili hao walizungumza mjini Nanyuki katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa soko la kisasa.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *