OWINO AAPA KUUNGUSHWA MSWADA

Huku mswada wa fedha wa mwaka wa 2024-25 ukitarajiwa kuwasilishwa bungeni muda wowote kuanzia sasa, mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, amewataka wabunge wanaoegemea mrengo wa Azimio kuungusha mswada huo licha ya mependekezo kadhaa kuondolewa.
Akizungumza na wanahabari, Owino amesema kuwa Kenya ianategemea pakubwa bidhaa zinazoagiwa kutoka mataifa ya kigeni, na hivyo ushuru unaopendekezewa bidhaa hizo utaendelea kuwa mzigo kwa wakenya.
Baadhi ya bidhaa hizo ni mayai, vimbaka na karatasi shashe.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa