#Athletics #Sports

TEAM KENYA YAJIANDAA KWA MBIO KULE GUANGZHOU

Timu ya Kenya inakamilisha mazoezi yake ya makazi leo katika Uwanja wa Ulinzi Sports Complex kabla ya Mashindano ya Dunia ya Mbio za kupokezana kijiti mjini Guangzhou, Uchina, Mei 10-11. 

Timu hiyo ilipiga kambi katika uwanja huo wa kijeshi siku mbili tu baada ya mchujo wa kitaifa Aprili 11-12 ingawa walikuwa wakitembelea msitu wa Karura kwa mazoezi ya asubuhi kwa siku maalum.

Timu inaondoka leo saa kumi na mbili na dakika 10 jioni kwa ndege ya kupitia Doha hadi UChina Alhamisi alasiri. 

Kocha Stanley Towet anatumai watatumia vyema siku zao za mazoezi magumu watakaposhindana katika Makala ya saba ya mashindano hayo ya kimataifa kwani ameona maboresho ya ajabu katika wanariadha wake.

Bingwa wa Michezo ya Jumuiya ya Madola katika mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala, Mwana Olimpiki Zablon Ekwam na kocha Simon Riga tayari wako nchini China kama sehemu ya kikosi cha Kenya kilichofika mapema. 

Huku hayo yakijiri, bingwa wa dunia wa mbio za mita 800 Mary Moraa atakosa michuano hiyo kutokana na tatizo la visa.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *