UKOMBOZI WA MACHOZI KWA RONALDO KWENYE ‘EURO ZA MWISHO

Ukombozi Wa Machozi Kwa Ronaldo Kwenye ‘Euro Za Mwisho”
Mkono wa Jan Oblak ulipopenyeza penalti ya muda wa ziada ya Cristiano Ronaldo kwenye nguzo, ndoto za nguli huyo wa Ureno zilikatizwa kwa muda mfupi.
Penalti ya Ronaldo iliokolewa katika muda wa nyongeza na mechi ya hatua ya 16-bora bila bao, lakini dakika 15 baadaye alipanda eneo lile lile na kupiga mikwaju ya kwanza ya nchi yake.
Kipa Diego Costa kisha aliweka historia ya michuano ya Euro kwa kuokoa mikwaju mitatu ya penalti huku Ureno ikinusurika kutolewa kwa njia ya aibu, na kuwashinda Slovenia na kupanga mechi ya robo fainali na Ufaransa.
Imetayarishwa na Janice Marete