#Sports

MURUNGA AKASHIFU MIZOZO YA RAGA

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Kenya Harlequins Paul ‘Pau’ Murunga amekashifu mizozo ya uongozi inayokebehi Muungano wa Raga ya Kenya akisema ni matokeo ya ubinafsi na uchoyo.

Pau hakughairi maneno yake alipokuwa akitoa tathmini kali kwa bodi ya sasa ya wakurugenzi wa Muungano huo, akisema wengi wao wamekaa kupita kiasi katika nyadhifa zao.

Mchezaji huyo wa zamani wa Shujaa kwa sasa ametoa changamoto lwa damu change katika mchezo huo kujitokeza na kutafuta nafasi kutoka kwa vilabu vyao, kama njia ya kupanda daraja hadi kwenye bodi.

Pau sasa anatoa wito wa kuvunjwa kabisa kwa bodi ya sasa na kuruhusu uchaguzi mpya.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MURUNGA AKASHIFU MIZOZO YA RAGA

NITABADILISHA AFC ASEMA AMBANI

MURUNGA AKASHIFU MIZOZO YA RAGA

MBOYA AJIVUNIA KUSHINDA TAJI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *