SHIF NI HARAMU

Mahakama Kuu imetangaza Bima ya Afya ya Jamii SHIF kuwa kinyume na katiba.
Wakati wakitoa uamuzi wao, Majaji Alfred Mabeya, Robert Limo na Friday Mugambi wameipatia Bunge makataa ya siku 120 kufanya marekebisho ya Sheria hiyo.
Jopo la majaji watatu limesema bunge linapaswa kushiriki ipasavyo kwa wananchi kwa mujibu wa katiba kabla ya kutunga sheria hiyo hiyo na kufanya marekebisho ya vifungu vinavyokiuka katiba.
Imetayarishwa na Janice Marete