POLISI WALIOMJERUHI MCHUUZI KUSALIA NDANI KWA SIKU 15
Polisi 2 waliokamatwa baada ya kuonekana wakimpiga na kumjeruhi mchuuzi mmoja hapa Nairobi wakati wa maandamano watasalia ndani hadi tarehe 3 mwezi Julai.
Mahakama imeagiza wawili hao Barasa Masinde na Dancun Kiprono kuendelea kuzuiliwa kwa muda wa siku 15 ili kutoa nafasi ya kukamilishwa kwa uchunguzi dhidi yao.
Wawili hao walimjeruhi mchuuzi Bonface Mwangi Kariuki ambaye amelazwa katika hospitali ya Kenyatta katika chumba cha wagonjwa mahtuti.
Imetayrishwa na Maureen Mukhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































