MAHAKAMA YAHARAMISHA NYONGEZA YA KODI
Mahakama kuu ya Mombasa imesitisha utekelezaji wa nyongeza ya kodi ya ukarabati barabara inayotozwa kwa bidhaa za kawi iliopaswa kuanza kutekelezwa tarehe 15 mwezi jana.
Jaji wa mahakama hiyo Gregory Mutai ametoa agizo hilo wakati mamlaka ya barabara kuu nchini Kenya imetoa taarifa ikiwaeleza wakenya umuhimu wa kodi hiyo ikiwemo kuimarisha ubora wa barabara.
Hata hivyo, uamuzi wa mahakama unamaanisha kwamba nyongeza ya shilingi 8 kwa lita ya petroli haitatekelezwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































