RUTO AZINDUA KITUO CHA SARATANI KISII
Rais William Ruto amezindua rasmi ujenzi wa kituo kikuu cha matibabu ya magonjwa ya saratani mjini Kisii, ujenzi huo ukiratibiwa kugharimu shilingi bilioni 3.2.
Kwa mujibu wa Rais, ujenzi huo utakamilika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja unusu ili kuwapa wakenya nafuu kuhusiana na gharama ya matibabu ya saratani.
Rais amezindua ujenzi huo alipokuwa kwenye siku yake ya pili ya ziara katika kaunti za Kisii na Nyamira.
Wakati uo huo, Rais amewapuzilia mbali wanaokosoa ushirikiano wake na chama cha ODM.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































