KANJA AAPISHWA KUWA INSPEKTA MKUU WA POLISI

Uongozi wa idara ya polisi umeimarika baada ya Douglas Kanja kuapishwa na kuanza majukumu yake rasmi kama inspekta mkuu wa polisi, na kujaza rasmi pengo lililoachwa na mtangulizi wake Japheth Koome.
Hafla ya kumuapishwa imefanyika katika mahakama ya upeo jijini Nairobi, muda mfupi baada ya Rais William Ruto kumteua.
Kanja atahudumu kwenye wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 4.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa