WAWILI MAHAKAMANI KWA UFUJAJI WA FEDHA WEST POKOT

Maafisa wawili wa zamani katika serikali ya kaunti ya West Pokot wanatarajiwa kufikishwa katika mahakama jijini Eldoret kufunguliwa mashtaka ya ufujaji wa shilingi milioni 296 zilizokuwa zimetengewa hazina ya ufadhili wa masomo.
Wawili hao waliokamatwa na tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC, walihojiwa hapo jana na kuzuiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini humo.
Msemaji wa EACC Eric Ngumbi, tume hiyo inawasaka washukiwa wawili zaidi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa