MSHTUKO MIILI 9 IKIPATIKANA MUKURU

Wenyeji katika mtaa wa Mukuru jijini Nairobi waemachwa na mshtuko baada ya miili 9 ya binadamu kupatikana kwenye shimo moja baadhi ikiwa imekatwakatwa karibu na kituo cha polisi cha Kware mtaani humo.
Kamanda wa polisi kaunti ya Nairobi Adamson Bungei, amesema miili 8 ni ya kike, huku akisema uchunguzi umeanzishwa.
Miili hiyo imepatikana na kundi la vijana eneo hilo, na imepelekwa katika hifadhi ya City.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa