UPINZANI WAMTAKA MURKOMEN NJE
Viongozi wa upinzani Kalonzo Musyoka na Eugene Wamalwa wanashinikiza kujiondoa afisini kwa waziri wa usalama Kipchumba Murkomen kufuatia kifo cha mchuuzi Boniface Kariuki aliyefariki kutokana na jeraha la risasi kichwani.
Wakizungumza baada ya kuitembelea familia hiyo, viongozi hao wamekariri kuwa Murkomen anafaa kuwajibikia kifo hicho.
Familia hiyo kwa sasa anaendeleza mipango ya mazishi ya jamaa yao.
Imetayarishwa na Tonny Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































