VIONGOZI WAMLILIA RAILA KUHUSU IRENE MASIT

Viongozi kutoka kaunti ya Elgeyo Marakwet wanamwomba kiongozi wa ODM Raila Odinga kuingilia kati na kuhakikisha kwamba aliyekuwa kamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Irene Masit anarejea nyumbani kutoka mafichoni.
Viongozi hao wamezungumza kwenye hafla ya mazishi ya babake Masit Mzee Chirchir Masit katika eneo la Chepkorio kaunti hiyo, ambako Odinga vile vile amehudhuria.
Viongozi hao wakiwemo wabunge wa zamani, wamemtaka Odinga kutumia uhusiano mwema alio nao na Rais William Ruto kumsaida Masit kureja nyumbani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa