#Local News

EACC YAWAKAMATA MAAFISA WAWILI WA TRAFIKI KERICHO KWA MADAI YA KUCHUKUA HONGO

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imewakamata maafisa wawili wa polisi wa trafiki kwa madai ya kukusanya hongo katika eneo la Litein mjini, kando ya barabara ya Sotik-Kericho.

Ikithibitisha kukamatwa kwa watu hao Tume hiyo kupitia kwa Msemaji wake Eric Ngumbi, imesema kuwa imeingilia kati kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa umma

EACC ilisema kumekuwa na malalamishi kwamba maafisa wa polisi wa trafiki katika barabara ya Sotik-Kericho wanadaiwa kuwaibia madereva na umma pesa kwa kisingizio cha utekelezaji wa sheria za trafiki, hivyo basi kuchangia ajali za barabarani.

Washukiwa hao wameachiliwa kwa dhamana wakisubiri kukamilika kwa uchunguzi.

Imetayarishwa na Janice Marete

EACC YAWAKAMATA MAAFISA WAWILI WA TRAFIKI KERICHO KWA MADAI YA KUCHUKUA HONGO

RUTO AANZISHA MCHAKATO WA KUBUNI IPOA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *