MIAMBA WA RAGA KENYA KWENYE NUSU FAINALI RAGA
Shule ya upili ya All Saints ya Embu imeratibiwa kumenyana na wenzao Kitondo katika semi fainali za raga ya wachezaji 15 kila upande katika mashindano yanayoendelea ya shirikisho la shule za upili ukanda wa Afrika nchini Uganda.
All saints ambao ndio mabingwa wa Kenya, walifuzu kwenye fainali baada ya kumaliza kileleni mwa kundi lao bila kupoteza, wakiicharaza Namilyango 13-7 katika mchuano wao wa mwisho.
Wakati huo uo, Kitondo ambao wanatokea katika kaunti ay Makueni, waliichabanga Kings College 24-11 na kumaliza wa pili katika kundi lao na kuweka miadi na All Saints.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































