#Business

KENYA MBIONI KUMALIZA EUROBOND

Kenya imelipa dola milioni 556.97 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 71.5 zilizosalia za Eurobond ya dola bilioni 2 kiwango sawa na shilingi bilioni 257 ambazo zilipaswa kulipwa kufikia leo.

Takwimu za Ofisi ya Kusimamia Madeni ya Umma ya Hazina ya Kitaifa zinaonyesha kwamba deni hilo ambalo lilikuwa limesalia lilipwa siku ya ijumaa iliyopita siku tatu kabla ya tarehe iliyoratibiwa.

Malipo hayo yamefanya hifadhi ya kitaifa kupanda juu ya mahitaji ya kisheria ya miezi minne kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi mitano.

Mwezi Februari, Kenya ilipata nafuu kwa kiasi fulani na kuingia sokoni na toleo jipya.

Serikali ilipokea zabuni zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.48 na ilikubali zabuni halali za jumla ya Dola za Marekani bilioni 1.44.

Awali Kenya ilikuwa imedokeza kwamba kiasi kilichosalia kingekamilishwa kupitia  ufadhili wa kimataifa na wa ndani.

Hazina ya Kitaifa mwezi Februari mwaka huu, ilithibitisha kuwa nchi hii ilifanikiwa kutoa Eurobond mpya na mipango ya kununua tena ile ya kwanza iliyotarajiwa kulipwa leo hii.

Hazina alisema mkopo mpya ambao ulikusudiwa kukamilisha Eurobond inayoendelea kukomaa umegawanywa katika awamu tatu, na maisha ya wastani ya uzani wa miaka sita, na unatarajiwa kukomaa mwaka wa 2031.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

KENYA MBIONI KUMALIZA EUROBOND

WITO WA KRA

KENYA MBIONI KUMALIZA EUROBOND

“IMFIKIE INJENDI!”- WAANDAMANAJI MALAVA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *