MWUGUZI MAKUENI ACHUNGUZWA KWA ‘KULIPIZA KISASI’
Serikali ya kaunti ya Makueni inachunguza tukio ambapo mwuguzi mmoja anadaiwa kudinda kumhudumia mwanamke aliyetaka kujifungua katika kituo cha matibabu cha Mavinye Little Dispensary na kumlazimu mwanamke huyo kusaka huduma za mkunga wa kienyeji licha ya serikali kuendeleza kampeni za kuwataka akina mama wajifungulie hospitalini.
Kulingana na Tabitha Mutuku ambaye ni mama mkwe wa mwanamke huyo, mwuguzi huyo alikataa kumhudumia mwanamke huyo kwa misingi kwamba aliwahi kumripoti kwa wakubwa wa afya kwamba alikuwa akimpa dozi za dawa zisizokamilika.
Waziri wa afya kwenye serikali ya kaunti hiyo Daktari Paul Musila, amekiri kupokea malalamishi hayo na kwamba hatua mwafaka zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































