LIPA UHURU PESA ZAKE; MAKUENI SENETA AMWAMBIA RUTO

Seneta wa makueni Dan Maanzo ameelekeza kidole cha lawama kwa serikali nkwa kukosa kufadhili shughuli za ofisi yar ais mstaafu Uhuru Kenyatta akisema kuwa hatua hiyo ni kumkosea heshima.
Maanzo aidha ameongeza kuwa rais William Ruto anafanya hivyo kulipiza kisasi kufuatia msimamo wa uhuru wa kisisasa katika uchaguzi uliopita.
Seneta wa Muranga Joe Nyutu kwa upande wake amesema kuwa pana haja ya serikali kufanya mazungumzo na ofisi ya Kenyatta kabla ya kuchukua hatua zinazolemaza shughuli zake.
Imetayarishwa na Janice Marete