ONYO YA AFISI YA DETA KWA WAKENYA
Afisi ya msimamizi wa deta imewaonya wakenya dhidi ya kuweka wazi maelezo ya kibinafsi ya wenzao, zikiwemo nambari za simu, baada ya baadhi ya Wakenya katika mitandao ya kijamii kuweka wazi nambari za simu za wabunge na viongozi wakuu serikalini kwa lengo la kuwashinikiza kuangusha mswada wa kifedha.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, afisi ya deta imesema hatua hiyo inakiuka kipengee cha 31 cha katiba na sheria ya ulinzi wad eta ya mwaka 2019.
Kwa mujibu wa afisi hiyo, baadhi ya maelezo yaliyowekwa wazi ni majina, nambari za simu, mahali wanakoishi na maelezo ya familia zao, wakitaka walioathirika kuwasilisha malalamishi kwa afisi hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































