#Sports

CHELSEA WAWABWANGA FLUMINENSE

The mighty Blues Chelsea ilitinga fainali ya Kombe la Dunia la Klabu huku mabao mawili ya mchezaji mpya Joao Pedro yakisaidia kuzamisha Fluminense ya Brazil.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, akicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya klabu yake ya utotoni, alipachika bao la kwanza dakika ya 18 baada ya mlinzi wa zamani wa The Blues Thiago Silva kushindwa kuondoa krosi ya Pedro Neto.

Chelsea wakionekana kucheza dhidi ya ulimwengu wote walijinasua kupitia kwa Kombora la pili la pedro katika dakika ya 56,ambalao lilisaidia kuwazamisha na kuwanyamazisha fluminense ambao walikua wamepigiwa upato mkubwa sana na mashabiki wengi

Ushindi huo unaihakikishia Chelsea kuongeza pauni milioni 22 kwenye pauni milioni 60 ambazo tayari zimepatikana kwenye michuano hiyo, huku Joao Pedro akisaidia haraka kulipa baadhi ya pauni milioni 55 zilizolipwa kumsajili kutoka Brighton wiki iliyopita.

The Blues watamenyana na Real Madrid au Paris Saint-Germain katika fain

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *