KOOME ATAKA USHIRIKIANO KUKOMESHA DHULUMA ZA KIJINSIA

Katika juhudi za kumaliza dhuluma za kijinsia, Wakenya wametakiwa kushirikiana na mahakama na mashirika ya serikali kukabili ongezeko la visa hivyo.
Jaji Mkuu Martha Koome amesema dhuluma za kijinsia ni janga la kijamii na zinaweza kutokomezwa tu kwa ushirikiano wa jamii na taasisi husika.
Akizungumza mjini Kisumu wakati wa uzinduzi wa mahakama maalum ya kushughulikia kesi za aina hiyo, Koome amesema maeneo kama Kisumu ni miongoni mwa vituo vya dharura kutokana na visa vingi vya ukatili huo huku akisisitiza kuwa haki kwa makundi yaliyo hatarini haipaswi kupatikana mahakamani pekee bali kupitia msaada mpana wa jamii.
Imetayarishwa na Janice Marete