TEUZI NNE ZA RUTO ZAPATA PIGO

Serikali imepata pigo baada ya uteuzi wa hivi majuzi wa maafisa wanne akiwemo Philip Kirua ambaye aliteuliwa kuwa afisa mkuu mtendaji wa Hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi.
Wengine ambao wameadhiriwa na uamuzi huo ni akiwemo meneja mkurugenzi wa shirika la habari la KBC Agnes Kalekye ambaye uteuzi wake umesitishwa hadi kesi iliyowasilishwa itakaposikilizwsa na kuamuliwa.
Hakimu Samuel Muochi ametoa uamuzi huo ambao pia umefutilia mbali uteuzi wa Joseph Kamau kuwa afisa mkuu mtendaji wa mamlaka ya maendeleo ya mto athi na Abdala Hatimia ambaye aliteuliwa kuwa afisa mkuu mtendaji wa taasisi ya kenya national shipping line limited.
Kesi ya kupinga uteuzi huo iliwasilishwa na dkt Magare Gikenyi na wanaharakati wengine watano ambao wameutaja kuwa kinyume na sheria .
Imetayarishwa na Janice Marete