#uncategorized

EACC YAKANA KUTUMIWA KISIASA

Mwenyekiti wa tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC David Oginde amekanusha madai ya baadhi ya wanasiasa kwamba tume hiyo hutumiwa kisiasa.

Oginde amesema  tetesi hizo huibuka hasa taifa linapokaribia uchaguzi mkuu, ambapo washukiwa hulaumu serikali ama upinzani wanapokamatwa ama kuagizwa kufika mbele ya tume hiyo.

Amekariri kwamba kesi ambazo huwasilishwa na tume hiyo huwa na Ushahidi dhabiti na wala hazitumiki kumgandamiza mtu yeyote.

Oginde amesema haya katika kikao na wanahabari baada ya uzinduzi wa ripoti ya matukio ya mwaka wa kifedha 2022-23.

Kwa upande wake, afisa mkuu mtendaji Twalib Mbarak ameshangaa ni vipi washukiwa wanaodai kuhangaishwa kisiasa, huwatuma wajumbe katika makao makuu ya tume hiyo kuomba washukiwa walegezewe kamba.

Aidha, Mbarak amesema pana haja ya ushirikiano ili kukabiliana na ufisadi kikamilifu.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *