WATU WENYE SILAHA WAUA MTU, NA KUIBA NG’OMBE 100 HUKO ISIOLO
Polisi wanasaka Kundi la watu wenye silaha ambao wamevamia kijiji cha Isiolo na kumuua mchungaji mmoja kabla ya kutoroka na ng’ombe 100.
Kulingana na Polisi uvamizi huo umefanyika usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kambi Garba.
Genge hilo limempiga risasi mchungaji mmoja kifuani walipovamia boma na kumuua papo hapo kabla ya kuondoka na ng’ombe waliokuwa kwenye boma.
Eneo hilo ni miongoni mwa maeneo ambayo bado yanakabiliwa na tishio la wizi wa mifugo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































