MAHAMAKA YA MAVOKO IMECHOMEKA
Maafisa wa polisi katika kaunti ya Machakos wameanzisha uchunguzi baada ya faili kadhaa za kesi kuchomeka kufuatia moto kuzuka usiku wa kuamkiia leo katika mahakama ya Mavoko.
Inaarifiwa kuwa moto huo umezuka katika maktaba ya mahakama hiyo kabla ya kusambaa hadi katika ofisi za hazina ya mahakama hiyo.
Maafisa wa polisi wa athi river wakishirikiana na wenzao wa zima moto wa kaunti ya Machakos wameweza kuudhibiti moto huo huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijabainika.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































