HATMA YA JOPO LA MAJAJI 3 KUBAINIKA

Naibu rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua ameratibiwa kuwafahamu majaji watakaosikiliza kesi inayolenga kuondoa maagizo ya kumzuia naibu rais mteule Kithure Kindiki kuanza majukumu yake, wakati jopo la majaji 3 litatoa uamuzi wa iwapo watajiondoa kwenye kesi hiyo au la.
Majaji hao ambao ni Anthony Mrima, Eric Ogola na Frida Mugambi wameratibiwa kutoa uamuzi huo alasiri hii.
Haya yanajiri baada ya mawakili wa Gachagua kushikilia kwamba naibu jaji mkuu Philomena Mwilu hana mamlaka kisheria kubuni jopo la majaji.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa