GAVANA MUTAI AKODOLEA HOJA YA KUTIMULIWA

Huenda gavana wa kaunti ya Kericho Eric Mutai akabanduliwa kutoka mamlakani baada ya wawakilishi wadi kwenye kaunti hiyo kutishia kuwasilisha mswada wa kumbandua hii leo kutokana na madai ya utumizi pesa za umma na ukiukaji wa sheria.
Wakiongozwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge la kaunti hiyo Philip Rono, wawakilishi wadi hao wamelalamikia kupungua kwa mapato ya kaunti hiyo, wakisema serikali hiyo imekusanya shilingi milioni 359 pekee katika mwaka uliopita wa kifedha, ikilinganishwa na shilingi bilioni 1.2 zilizolengwa na serikali hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa