#Business

CBK YAPUNGUZA RIBA YA MIKOPO

Ni afueni kwa mkopaji baada ya benki kuu ya kenya CBK kupunguza viwango vya riba vya mikopo kutoka asilimia 10 hadi asilimia 9.75 ili kuchochea utoaji mikopo kwa sekta ya binafsi.

Gavana wa CBK Kamau Thugge aliyeongoza mkutano wa Kamati ya Sera ya Fedha jijini Nairobi, amesema kulikuwa na wito wa kurahisisha zaidi sera ya fedha ili kuongeza hatua za awali za sera zinazolenga kuchochea ongezeko la mikopo inayotolewa na benki za biashara kwa sekta ya binafsi, na kusaidia shughuli za kiuchumi.

Thugge aidha amesema mfumuko wa bei wa jumla unatarajiwa kuendelea kuwa chini ya asilimia 5.0 ya kiwango cha lengo la katikati katika muda mfupi ujao, akitaja kuwa benki kuu itafuatilia kwa karibu athari za uamuzi wa sera pamoja na maendeleo katika uchumi wa dunia na wa ndani, na iko tayari kuchukua hatua zaidi zinazohitajika.

Imetayarishwa na Maureen Amwai

CBK YAPUNGUZA RIBA YA MIKOPO

MKATABA WA SERIKALI-ADANI MAHAKAMANI

CBK YAPUNGUZA RIBA YA MIKOPO

RAIS ASHTUMU KIFO CHA OJWANG

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *