ARSENALI WATANGAZA KIKOSI CHA MICHEZO YA URAFIKI

Klabu Ya Soka Ya Uingereza, Arsenal Inawakosa Wachezaji Wake Muhimu Bukayo Saka, Kai Havertz, Declan Rice, William Saliba, Gabriel Magalhães Na Gabriel Martinelli Wanaposafiri Kuelekea Marekani Kwa Ajili Ya michezo Yao Ya Kabla Ya Msimu Mpya.
Klabu Hiyo Yenye Maskani Yake Jijini London Wiki Hii Itaanza michezo Yao Ya Maandalizi Kabla Ya Msimu Wa EPL Wa 2024/25 Itakayoanza Mwezi Ujao.
Katika Taarifa Yake Jumapili, Klabu Hiyo Ilitangaza Kikosi Cha Wachezaji Ishirini Na Sita, Wakiwemo Vijana Wengi Ambacho Kitakuwa Marekani Kwa Ajili Ya Michezo Ya Maandalizi.
Klabu Hiyo Ilitangaza Kuwa Kutokana Na Maendeleo Yao Katika Michuano Ya Copa America Na Euro, Gabriel Magalhaes, Gabriel Martinelli Na Kai Havertz Watajiunga Na Kikosi Hicho Kuanzia Julai 25.
Wachezaji Walioshiriki Katika Hatua Za Mwisho Za Euro 2024 – Declan Rice, Aaron Ramsdale, Bukayo Saka, David Raya Na William Saliba – Wataungana Na Wenzao Watakaporejea Kutoka Amerika.
Mabeki Kieran Tierney Na Takehiro Tomiyasu Watasalia Jijini London Kupokea Matibabu Kutoka Kwa Wahudumu Wetu Wa Afya Huku Wakipambana Na Majeraha Ya Msuli Wa Paja Na Goti Mtawalia.
Katika Ziara Yao Ya Marekani, Wanabunduki Wanatarajiwa Kucheza Dhidi Ya Manchester United Julai 27, Liverpool Julai 31, Bayer Leverkusen Agosti 7 Na Olympique Lyonnais Agosti 11.
Imetayarishwa na Nelson Andati