IPOA YATISHIA KUELEKEA MAHAKAMANI

Mamlaka ya kutathmini utendakazi wa Polisi (IPOA) inataka kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja na Kamanda wa Polisi wa Nairobi Adamson Bungei wakamatwe kutokana na mienendo yenye kutiliwa shaka ya polisi iliyoshuhudiwa wakati wa maandamano ya nchi nzima.
Kamishna wa IPOA John Waiganjo amesema kwamba mamlaka hiyo inasikitishwa na ukosefu wa taaluma unaoonyeshwa na maafisa wa polisi wanapowahusisha waandamanaji katika muda wa wiki nne zilizopita na sasa wanazidisha suala hilo katika Mahakama.
Imetayarishwa na Janice Marete