MWAURA: SERIKALI INAIMARISHA KILIMO MAGHARIBI

Huku taifa likijiandaa kwa maadhimisho ya sherehe za 61 za Madaraka hapo kesho ambayo kauli mbiu yake ni kilimo na utoshelezi wa chakula, serikali imetambua eneo la Magharibi mwa nchi kama lenye uwezo wa ukulima, kutokana na mazao mbali mbali yanayozalishwa nae neo hilo.
Akiwahutubia wanahabari katika jumba la Nyayo jijini Nairobi, msemaji wa serikali Isaac Mwaura amesema serikali imeweka mikakati mwafaka kuhakikisha kuwa eneo hilo linaendelea kunawiri katika sekta ya kilimo.
Aidha, Mwaura ameelezea matumaini ya serikali kwamba eneo hilo litainuka kiuchumi kutokana na kuwa wenyeji wa sherehe za Madaraka.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa.