AFISA WA IEBC AKAMATWA KWA MADAI YA KUGHUSHI VYETI VYA MASOMO
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imemtia mbaroni afisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) baada ya kudaiwa kutumia vyeti ghushi vya masomo kupata ajira katika bodi ya uchaguzi kuanzia Aprili 4, 2012.
Msemaji wa EACC Eric Ngumbi amesema kuwa Caroline Sabiri Manyange, Meneja wa Uwekaji Mipaka, amekamatwa nyumbani kwake Nairobi Magharibi na anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha EACC Integrity Center ambako.
Tume hiyo imebaini kuwa uchunguzi wao umefichua kuwa Caroline alighushi cheti cha shahada ya Uzamili ya Sanaa (Masomo ya Idadi ya Watu) kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi kilichotolewa Mei 9, 2004, na kukitumia kupata cheo katika tume ya IEBC.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































