KENYA YAAMRISHWA KUMFIDIA MWANAHABARI WA PAKISTAN
Mahakama kuu mjini Kajiado imeiagiza serikali ya kenya kuilipa shilingi milioni 10 familia ya mwanahabari Arshad Sharif raia wa Pakistan aliyuawa kwa kupigwa risasi hapa nchini mnamo mwezi Oktoba mwaka jana.
Akitoa uamuzi huo, hakimu Stella Mutuku amesema hatua ya kutumia nguvu na kumpiga risasi kichwani mwanahabari huyo ilikuwa kinyume na sheria .
Aidha, amemkosoa mwanasheria mkuu, afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma na idara nyingine za uchunguzi kwa kuzembea katika kukamilisha uchunguzi na kuwafungulia mashtaka maafisa wa polisi wanaohusishwa na mauaji ya mwanahabari huyo
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































