#Local News

KUNANI KATIKA CHAMA CHA UDA?

Malumbano ndani ya chama cha UDA yamechukua mkondo mwingine wakati ambapo bodi ya uchaguzi ya chama hicho ikifutilia mbali taarifa iliyokuwa imetolewa na katibu mkuu wa chama hicho Cleophus Malala kuahirisha uchaguzi ambao umepangiwa kufanyika katika kaunti 10 leo hii.

Mwenyekiti wa bodi hiyo Antony Mwaura anasema uchaguzi huo utaendelea jinsi ilivyoratibiwa katika kaunti za nairobi, pokot magharibi, narok, busia,,homa bay

Kwa mujibu wa Mwaura uamuzi wa awali wa baraza la chama la kutatua mizozo iliyomzuia Malala kuingilia uchaguzi wa chama akimkosoa kwa kile ametaja kua kukosa heshima kwa bodi ya uchaguzi wa chama hicho.

Mkanganyiko huo unajiri wakati ambapo tofauti zinaendelea kuonekana wazi ndani ya chama hicho.

Mvutano uliibuka wakati ambapo Malala aliwaonya wabunge dhidi ya kuwakosea heshima viongozi wakuu chamani akisema wataadhibiwa.

Imetayarishwa na Janice Marete

KUNANI KATIKA CHAMA CHA UDA?

AZIMIO WAKOSOA MSWADA WA FEDHA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *