ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUMKATA JIRANI YAKE MKONO
Mvulana mwenye umri wa miaka 17 anauguza majeraha katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Siaya ambapo alikimbizwa baada ya kuokolewa kutoka mikononi mwa umati wenye hasira uliotaka kumuua katika kijiji cha Mahaya Kaunti ya Siaya.
Mtoto huyo aliokolewa na polisi baada ya wananchi kumshukia kwa madai ya kushambulia na kumkata mkono jirani yake Mariko Monye.
Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Siaya Cleti Kimaiyo, iliripotiwa katika kituo cha polisi cha Aram na Chifu Msaidizi wa eneo hilo Moses Ombewa kwamba mkono wa Mariko ulikuwa umekatwa na watu wasiojulikana.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































