OCHOLLA AJIVUNIA BAADA YA USHINDI MARA MBILI
Kocha mkuu msaidizi wa timu ya wanawake ya KPA Kenya Samuel Ocholla amepongeza hatua yake baada ya kusajili ushindi mara mbili wikendi.
The Dockers walipeana kichapo cha 84-38 dhidi ya The Swish Jumamosi kabla ya kupepeta The Storms 87-44 siku ya Jumapili katika Ukumbi wa Makande Gymnasium, Mombasa.
Licha ya mwendo mzuri, mtaalamu huyo anayezungumza kwa upole anaamini kazi bora zaidi haijaonekana kwa wasichana wanapojiandaa kwa mchujo.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































