BUNGE LAIDHINISHA WANAJESHI VICHOCHORONI

Bunge la kitaifa limeidhinisha hatua ya jeshi la KDF kutumwa ili kushirikiana na maafisa wa polisi kurejesha utlivu nchini baada maafa yaliyosabibishwa na maandamano ya kupinga mswada wa fedha.
Mswada huo ambao umewasilishwa na kiongozi wa walio wengi katika bunge hilo Kimani Ichung’wa na kupigiwa kura na wabunge, saa chache baada ya Waziri wa ulinzi Aden Duale kuchapisha kwenye gazeti rasmi la serikali kuhusu hatua ya kuwatuma wanajeshi kwenye operesheni hiyo.
Tayari wanajeshi wametumwa kushika doria katika maeneo ya kiserikali kwa hofu ya kushambuliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa