RUTO AOMBOLEZA KIFO CHA RAISI

Rais William Ruto amemwomboleza mwenzake wa Iran Ebrahim Raisi, aliyefariki katika ajali ya ndege hapo jana, Ruto akimtaja mwendazake kama mtu mwenye msimamo na asiye na uoga katika kutekeleza alichokiamini.
Kupitia ukurasa wake wa X awali ukifahamika kamaTwitter, Ruto ambaye yuko safarini kuelekea nchini marekani, vile vile amemkumbuka Raisi kama mtu aliyejitolea kuiweka Iran katika ramani ya ulimwengu, huku akijivunia uhusiano wake na mwendazake wakati wa uongozi wao.
Wakati wa ajali hiyo, Rais Ebrahim alikuwa na Waziri wa masuala ya kigeni Hossein Amir-Abdollahian na maafisa wengine wa kuu serikalini
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































