WAIGURU AAHIDI KUIMARISHA BIASHARA KIRINYAGA

Shughuli za biashara zimeratibiwa kurahisishwa katika kaunti ya Kirinyaga kufuatia mpango wa ujenzi wa soko la kisasa katika eneo la Kagio kwa ushirikiano wa serikali kuu na ile ya kaunti hiyo ili kupunguza msongamano.
Akizungumza katika mkutano eneo hilo, gavana Anne Waiguru amesema kuwa masoko 11 zaidi yatajengwa chini ya mpango wa kichecheo cha uchumi ili kuimarisha biashara kwenye kaunti hiyo.
Aidha, wakazi wameunga mkono ujenzi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa