SABABU FICHE YA KUMTIMUA MWANGAZA, WAKILI NJIRU
Wakili mkuu anayewakilisha bunge la kaunti ya Meru katika vikao vya kumbandua gavana Kawira Mwangaza kwenye bunge la seneti Ndegwa Njiru, ameiambia seneti kwamba kuna sababu fiche inayoashiria kwamba Mwangaza hana uwezo wa kuiongoza kaunti hiyo.
Wakili huyo amesema ni mara ya tatu sasa bunge la seneti limelazimika kuingilia kati kwa lengo la kubaini uwezo wake kuendesha kaunti hiyo, na hivyo umma kupoteza imani kwa gavana huyo.
Katika utangulizi wa mawasilisho yake, Njiru ameahidi kuwasilisha Ushahidi wa kuonyesha kauli za kiholela za gavana Mwangaza ambazo zimesambaratisha familia kadhaa kwenye familia hiyo.
Aidha, wakili huyo ameahidi kuwasilisha mashahidi katika madai yanayoashiria ukosefu wa uadilifu kwa gavana huyo inavyohitajika kikatiba kwa afisa wa umma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































