APOSTLE MANYURU AONGOZA UZINDUZI WA PVK NAIROBI

Muungano wa makanisa ya Kipentekote yamezindua rasmi muungano wao wa Pentecostal Voice of Kenya ukanda wa Nairobi, katika hafla ya kufana ambayo imeandaliwa katika ukumbi wa kanisa la Jesus Teaching Ministry ama JTM kwenye jumba la Kahawa jijini Nairobi.
Hafla hiyo imeongozwa na mwenyekiti wa muungano huo ambaye pia ni mwanzilishi wa kanisa la JTM Apostle Peter Manyuru, akisema kwamba lengo la muungano huo ni kuhakikisha kwamba wachungaji na wakristo wanatekeleza majukumu yao kwa kujiamini, mbali na kuimarishwa kiuchumi.
Aidha, Apostle Manyuru amewahimiza wanachama kukumbatia umoja, ili kuafikia malengo ya muungano huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa