KUNDI LA WAKENYA LAELEKEA MOSCOW KWA AJIRA

Kundi la wafanyikazi 50 raia wa Kenya waliondoka nchini wiki jana kwa fursa za ajira nchini Urusi, kuashiria mwanzo wa mpango mpya wa uhamiaji wa wafanyikazi unaolenga kushughulikia ukosefu wa ajira kwa vijana.
Kundi hilo, linalowajumuisha watu kutoka kaunti mbalimbali, linatarajia kufanya kazi katika kiwanda cha kupakia chakula nje ya jiji la Moscow. Kulingana na maafisa, waajiriwa watapata mshahara wa Sh115,000 kila mwezi na kupokea malazi na chakula bila malipo kutoka kwa mwajiri wao.
Uajiri huo uliwezeshwa na wakala wa Yumna wakisaidiwa na Uwezo Fund, ambao uligharamia tiketi za ndege na ada za upangaji kupitia mpango wa mkopo. Wafanyikazi wanatarajiwa kurejesha mkopo huo baada ya muda watakapoanza kulipwa nje ya nchi. Wakizungumza katika hafla ya kuwatuma kazini iliyofanyika Nairobi, wawakilishi wa serikali wamewataka wafanyikazi kuweka akiba na kuwekeza mapato yao nyumbani
Imetayarishwa na Maureen Amwai