KAMATI YA UTEUZI YAMKATAA MTEULE MMOJA
Kamati ya uteuzi katika bunge la kitaifa imekataa uteuzi wa Stella Soi kuhudumu kama Waziri wa masuala ya kijinsia, na kuwaidhinisha wateule wengine 19 waliopigwa msasa wiki jana.
Hatima ya Soi imo mikononi mwa bunge ambao wanatazamiwa kuona iwapo watamwidhinisha au kudumisha uamuzi wa kamati hiyo.
Kamati hiyo inatarajiwa kuwasilisha ripoti ya msasa bungeni muda wowote kuanzia sasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































