#Local News

SIMAMA NA FAMILIA YA REX MASAI

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amewataka Wakenya kusimama na familia ya Rex Kanyike Maasai, ambaye inasemekana aliuawa wakati wa maandamano ya jana Alham jioni.

Inasemekana kwamba Rex alipigwa risasi na kuuawa mwendo wa saa saba mchana katika barabara ya Moi avenue jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.

Akizungumza alipoungana na familia ya Rex katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City kabla ya upasuaji wa maiti, babu amesema amehuzunika kuona wazazi wakiwa katika majonzi kufuatia mkasa huo.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *